Habari za Punde

Wastaafu Waiomba PSSF Kulipa Fedha Zao Kwa Wakati.

 Na.Adeladius  Makwega - DODOMA

Watumishi waliostaafau na wale wanaokaribia kustaafu wameomba Serikali kuhakikisha inawalipa fedha zao ili kuwasaidia kuondoa malalamiko na matatizo ya kiafya yanayoweza kuibuka baada ya kustaafu.

 

“Mimi nimemaliza mafunzo ya kustaafu lakini ninayoyasikia kwa wezangu yananitia wasiwasi juu ya kupatikana kwa pesa zangu kwa wakati” anasema Bi Halima Mhina ambaye alikuwa Karani wa Masijala wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

Ni vizuri PSSF kulipa pesa hizo kwa wakati ili kila anayestaafu kupatiwa kilicho chake kwani hilo litaondoa malalamiko mioyoni, simanzi na kukata tamaa. kwa waliostaafu na wale wanaobaki kazini.

 

Tarehe ya kustaafu ya kila mtumishi inafahamika na kila upande hata PSSF, iweje tena malipo yachelewa? ni wajibu wa kila upande kutimiza wajibu wake mapema, aliongeza Bi Mhina .

 

“Mimi nimeondoka kazini tangu Februari 2021 lakini pia PSSF nayo imekuwa goigoi kuhusu malipo yangu unakuja kulipwa baada ya kadhaaz na jambo hili linafanya mtumishi hata kupata pesa yake ya mwezi inakuwa tabu, Je ataishije?” aliuliza Malima Ndelema ambaye aliwahi kufanya kazi kama Mtayarishaji Mwandamizi wa Vipindi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

 

Fedha hiyo si hisani bali ni haki ya mtumishi mstaafu kwa mujibu wa sheria na kama haki inachelewa maana yake ni kunyima haki yangu ya msingi, aliongeza Ndugu Ndelema. Kinachofanyika ni tafauti na wanayoyasema”Zilongwa mbali, Zitendwa mbali:”

 

Watumishi hao wamelalamikia muda wa mafunzo ya kustaafu kuwa ya muda mdogo kwani wengine wanatumia juma moja lakini taasisi zingine ni siku zaidi ya 21. Pia wameomba mafunzo hayo kutolewa hata kabla ya miaka mitatu nyuma ili mtumishi aweze kufanya majaribio ya yale mafunzo mapema.

 

Katika kila siku katika Utumishi wa Umma wapo watumishi wanaostaafu utumishi huo kwa hiari na kwa mujibu wa Sheria. Pia wapo watumishi wanaondoka kazini kwa kuacha kazi, kufukuzwa kazi na hata kufariki na PSSF wana wajibu wa kulipa fedha za wastaafu hao ambapo mtumishi na mwajiri wanachangia katika mfuko huo kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.