Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akitowa maelekezo kwa Mjenzi wa ukarabati wa Skuli ya Sekondari ya Ben Bella wakati alipotembelea Skuli hiyo kujionea maendelea ya ujenzi huo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said amefanya ziara kuangalia maendeleo ya matengenezo ya Skuli ya Sekondari Benbella yaliyoanza mwezi wa Novemba mwaka jana chini ya kampuni ya ujenzi MODERN BUILDING CONTRACTORS, ya hapa Zanzibar.
Mhe. Simai katika ziara hiyo amewataka wakandarasi wa ujenzi wa Skuli hiyo
Kuhakikisha matengenezo hayo yanakuwa bora na kumalizika kwa wakati.
Na Maulid Yussuf WEMA
No comments:
Post a Comment