Habari za Punde

Mufti Mkuu azitaka taasisi za kiislamu kufanya kazi kwa mujibu wa sheria

 

Na Takdir Suweid

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi  amezitaka taasisi za kiislamu nchini kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za usajili ili kuondosha mizozo na mifarakano miongoni mwao.

Akifunguwa mkutano Mkuu wa 20 wa  Taasisi ya kiislamu, elimu, uchumi na  maendeleo (UKUEM) kwa niaba yake  huko katika ukumbi wa Chuo Cha utalii Maruhubi sheikh Othman Mohammed Saleh amesema baadhi ya taasisi huanza migogoro wakati wanapopata maendeleo.

Amesema migogoro inasababisha kukwamisha maendeleo ya haraka katika nchi hivyo ni vyema kuacha majungu, fitna, uhasama na badala yake washirikiane katika kuendeleza mipango iliyopangwa serikali ya kuwaletea  maendeleo wananchi.

Hata hivyo amewataka kuitumia ofisi ya Mufti kwa kupata ushauri, elimu na masuala ya kijamii ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Wakitoa taarifa ya utendaji wa kamati za taasisi hiyo wamesema tokea kuanzishwa wamepata mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kusaidia vijana kwa kuwapatia mikopo ya kujiendeleza kielimu ili waweze kufikia malengo ya kupata elimu.

Mbali na hayo amesema licha ya kupata mafanikio hayo lakini wanakabiliwa na matatizo Kama vile ukosefu wa fedha za kuendesha miradi ya maendeleo wanayoianzisha na vitendea kazi Mambo ambayo yanakwamisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.