Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amezungumza na Kuwaaga Madaktari Bingwa wa Kichina Baada ya Kumaliza Muda wa Kazi Zanzibar.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Madaktari Bingwa  benchi ya 30 kutoka Nchini  China waliomaliza muda wao wa mwaka mmoja Zanzibar kutoka huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja na ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo ya kuwaaga imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, wa kwanza Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyika kazi  zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru kwa dhati Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa misadaa mbali mbali inayoendelea kuipatia Zanzibar, hususan katika sekta ya Afya.

Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo leo alipozungumza na Timu ya Madaktari kutoka China waliomaliza muda wao wa kazi, baada ya kuwepo nchini na kufanyakazi kazi katika Hospitali mbali mbali kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Amesema tangu kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, China imeendelea kuisaidia Zanzibar katika sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ikiwemo sekta za Afya; hususan katika uimarishaji wa miundombinu, upatikanaji wa vifaa, dawa pamoja na kuwajengea uwezo watendaji wa sekta hiyo.

Alisema katika kukabiliana na Ugonjwa wa Covid -19, China imeendelea kuisaidia Zanzibar katika utoaji  wa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya Afya  pamoja na wafanyakazi walioko katika sekta ya Utalii.

Aliiishukuru na kuipongeza Timu hiyo Madaktari kwa kuunga mkono juhudi za Serikali na kufanya kazi kubwa usiku na mchana ya kuwapatia huduma bora za Afya wananchi wa Zanzibar.

Katika hafla hiyo Rais Dk. Mwinyi alikabidhi zawadi kwa Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar, Zhnag Zhisheng pamoja na kuwavika nishani madaktari  hao.

Mapema, Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto Nassor Ahmeid Mazrui, alisema jamii haiwezi kuzungumzia Historia ya Zanzibar bila kuzingatia mchango mkubwa wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China, kupitia sekta mbali mbali kama vile Kilimo, Viwanda, miundombinu, Afya  na kadhalika.

Alisema timu ya Madaktari kutoka China iliomaliza muda wake wa kazi nchini katika Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja pamoja na Abdalla Mzee kisiwani Pemba imefanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kuwapatia wananachi  huduma bora, sambamba na kuwajengea uwezo w akiutendaji  madaktari wazalendo.

Alibainisha matarajio ya Wizara hiyo juu ya ujio timu mpya inayotarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni kuwa itaendeleza kazi ya utoaji wa huduma bora za Afya, ikiwa ni hatua ya kuendeleeza ushirkiano uliopo kati ya nchi hiyo na Zanzibar, ambapo utaratibu wa timu za Madaktari kutoka nchin hiyo kuja Zanzibar umekuwa ukifanyika kila mwaka.

Nae, Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar Zhang Zhisheng alisema Timu ya Madaktarihao kutoka China inafanyakazi chini ya miongozo ya Serikali ya China, ambapo katika kipindi hicho cha mwaka mmoja pamoja ilifanyakazi katika Hospitali za Mnazimmoja na Abdalla Mzee, Kivunge na Chakechake, ambapo katika siku za mwisho wa wiki Madaktari hao walifika vijijini kuwasaidia wananchi maskini walioshindwa kusafiri kufuata huduma za Afya mijini.

Alisema katika kipindi hiki Dunia ikikabiliana na ugonjwa wa Covid -19, China imesimama pamoja na wananchi wa Zanzibar katika kukabiliana na ugonjwa huo ili kuleta ustawi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aidha, Kiongozi Mkuu wa Madaktari kutoka China, Ms Dr Wang Yiming akitoa taarifa fupi ya kazi, alisema katika kipindi chote wawapo nchini walifanya kazi bega kwa bega na madaktari wazalendo na hivyo kufanikiwa kushinda changamoto mbali mbali ziliopo.

Alisemsa katika kipindi hicho walishughulikia kesi kadhaa za upasuaji pamoja na  kutembelea maeneo mbali mbali ya Zanzibar kwa ajili ya  huduma.  dawa pamoja na kuwaongezea uwezo wa kiutendaji  madakrai wenyeji.

Alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Afya, Jinsia na Watoto na wananchi wote wa Zanzibar kwa utii na kuiunga mkono timu hiyo, akibainisha matumaini makubwa ya timu ijayo kufanyakazi vyema kwa ajili ya Wazanzibari.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Jinsia na Watoto Fatma Mrisho alisema timu hiyo ni ya 30 ya Madaktari kutoka China, ambapo imefanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja katika Hospitali mbali mbali Unguja na Pemba.

Alisema katika timu hiyo kulikuwepo Madaktari katika fani mbali mbali, ikiwemo wa Upasuaji, X-Ray, Mionzi, huduma za watoto, magonjwa ya Moyo, Meno, tumbo kuchoma sindano za kupunguza hisia pamoja na wakalimani.

Alisema katika kipijndi hicho madaktari hao waliweza kufanyakazi zao kwa uborapamoja nakuongezeka ubora wa kiutendaji kwa madaktari waliopo nchini.

Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.