Habari za Punde

Serikali Kuanzisha Dawati la Habari Kila Balozi
 

Adeladius Makwega- WHUSM-Dodoma

 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanakusudia kuanzishwa kwa dawati la habari kwa Balozi zetu ughaibuni.

 

Wakilijadili suala hilo kwa kina wajumbe kutoka Wizara zote mbili wameona umuhimu wa kuanzishwa kwa dawati la habari katika Balozi hizo lli kuanzishwa kwa programu maalumu ya kutangaza Tanzania na kuibua fursa zilizopo katika mataifa mbalimbali duniari ambazo Balozi zetu zipo.

 

“Kunapaswa kuwepo na mfumo wa moja kwa moja kwa  Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali ili kupokea moja kwa moja habari za fursa kutoka Balozi zetu zote ng’ambo ili kuwajulisha wananchi na kuwavutia uwekezaji.” Amesema Nakomba Dahari Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki

 

Kikao hicho pia kimejadili na kukubaliana kwa kauli moja juu kuwepo na programu za kubadilishana kimafunzo kati ya Tanzania na mataifa mengine hilo linaweza kuongeza uwezo ili watumishi wa umma katika kada ya Habari waendelee kuboresha utendaji kazi wao uwe na tija kwa taifa kwa kuzingatia weledi wa taaluma yao.

 

“Kuanzishwa Makala na vipindi maaalumu vya utalii ili kuonesha fursa zote za utaliii, uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya kimkakati na fursa nyenginezo zilizopo nchi za nje zioneshwe katika runinga zetu.” Amesema Dkt. Emmanuel Temu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

 

Kikao hicho kimewajumuisha watendaji kadhaa wa Wizara hizo mbili huku sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zikitupiwa jicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.