Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii
leo Oktoba 12,2021 ametembelea mradi wa
ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere katika mto Rufiji, mradi unaogharimu shilingi
Trioni 6.58.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi
huo, Makamu wa Rais ameipongeza wizara ya Nishati, Wakandarasi pamoja na
wafanyakazi wote wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huo. Amesema mradi huo ni
mkombozi katika sekta ya nishati nchini hivyo amewataka viongozi na wote
wanaohusika katika mradi huo kuwa wazalendo na kutanguliza maslahi ya taifa
wakati wote.
Amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha
mradi huo unakamilika kama ilivyopangwa na hivyo ameagiza wakandarasi kuwa
makini na kutatuta hitilafu yeyote itakayojitokeza mapema ili kuepusha madhara
yanayoweza kujitokeza baadae katika mradi huo.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais
ameagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote inakopita mito inayotiririsha maji
katika mto Rufiji kutunza mito hiyo na kutoa elimu kwa wananchi ili kulinda
mazingira kwa manufaa ya mradi huo.
No comments:
Post a Comment