Habari za Punde

NRGI yashirikiana na ZAOGS kusaidia mchakato wa Mafuta na Gesi Zanzibar

 
Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Taasisi ya Utawala wa Rasilimali ya  Natural Resource Governance Institute (NRGI) imeeleza utayari wake wa kushirikisha na Serikali ya Zanzibar, sekta binafsi na asasi za kiraia kuunga mkono juhudi zinazoendelea kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali ya mafuta na gesi.

Mkurugenzi mwenza wa taasisi hiyo kanda ya Afrika, Silas Olang, alisema hayo wakati alipoitambulisha NRGI kwa Serikali, Sekta Binafsi na Asisi za Kiraia kufuatia mwaliko wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Zanzibar (ZAOGS).

“Tumekuja Zanzibar kuitambulisha NRGI kwa wadau  na kubainisha azma yetu ya kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha sekta hii inakuwa na manufaa kwa wananchi wa Zanzibar na Taifa,” alisema Silas.

Alisema uzoefu unaonesha sekta ya mafuta na gesi inakuwa na changamoto nyingi ikiwemo rushwa katika utoaji wa miakata, mgawanyo wa mapato yanayotokana na rasilimali hiyo, uharibifu wa mazingira kama hakutakuwa na udhibiti, migogoro ndani ya jamii ambayo inapaswa kushughulikiwa katika hatua za awali.

Katika majadiliano na wadau hao, Silas pia alifusia jinsi ya kutumia mapato yanayotokana na rasilimali hizo hasa katika uwekezaji katika maeneo mengine ya uchumi kwa sababu rasilimali hiyo inatumiwa na kumaliza.

Pia alizungumza jinsi ya kumanage expectation za wananchi, kutotumia utajiri wa mafuta kuingia kwenye madeni makubwa, kutumia vizuri mapato kwa sababu asilimia 90 ya nchi zinazozalisha rasilimali hizo wananchi wake ni masikini.

“Zaidi ya watu bilioni moja kutoka nchi zenye utajiri wa Mafuta ni masikini wa kutupwa kutokana na mgawanyo mbaya wa mapato yanayotokana na rasilimali hizi, kwa hivyo lazima tuchukue tahadhari na kujifunza makosa ya wengine,” alisema.

Alisema kwa kuwa NRGI ina uzoefu mkubwa katika sekta hiyo, iko tayari kushirilisha uzoefu wake kwa wadau wa Zanzibar ili kujiandaa kunufaika na rasilimali hizo.

Kwa unde wake, Muasisi na Mwenyekiti ZAOGS, Balozi wa Heshima wa Brazil nchini Tanzania, Abdulsamad Abdulrahmi  alielezea jinsi taasisi hiyo inavyojitolea kuhakikisha Zanzibar inanufaika na fursa mbali mbali za kiuchumi ikiwemo uchumi wa Mafuta na gaesi.

Alisema ZAOGS itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo NRGI kuhakikisha Zanzibar inafunguka kiuchumi katika kipindi kifupi kijacho.

“NRGI ni wadau muhimu kwa sekta hii hapa Zanzibar, tumishirikiana kuzijengea uwezo taasisi zinazoshughulika na extractive industry Tanzania Bara na sasa tumewaleta Zanzibar. Tunafanya hivi kuunga mkono malengo ya Rais wa Zanzibar, Dk, Hussein Mwinyi kuhakikisha Zanzibar inatimiza Ajenda yake ya Maendeleo ya 2050 na Malengo ya Dunia ya Maendeleo Endelevu (SDGs),” alisema Balozi.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.