Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameongoza Wananchi wa Mkwajuni Katika Dua Maalum Kuwaombea Waliotangulia Mbele ya Haki.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kuashiria kuanza kwa dua Maalum ya kisomo cha hitma kuwaombea waliotangulia mbele ya haki, dua iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mkwajuni Kidombo, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa, (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla  (kushoto kwa Rais) Mtoto wa Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Tano Alhaj. Dk.Salmin Amuor Juma.Ndg.Amini Salimin Amour.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja katika kisomo na dua Maalum kuwaombea Waliotangulia mbele ya haki, iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo, dua hiyo inayokwenda sambamba na Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman na (kushoto kwa Rais) Ndg. Amini Salimin Amour, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj.Othman Masoud Othman, Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj. Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
WANANCHI wa Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika dua Maalum na kisomo cha Hitma iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo, inayokwenda sambamba na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) hufanyika kila mwaka
VIONGOZI wa Serikali wakijumuika katika kisomo cha dua maalumu ya kuwaombea waliotangulia mbele ya haki katika Kijiji cha Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja dua iliyoendana na Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) wa kwanza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman, Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj.Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman. iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo,
WANANCHI wa Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika dua Maalum na kisomo cha Hitma iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo, inayokwenda sambamba na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) hufanyika kila mwaka 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.