Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Azindua Kampeni ya Uanaharakati Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi  Ali Khamisi (kulia)  wakati alipoingia kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam kuzindua  Kampeni ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika uzinduzi wa  Kampeni ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mwongozo wa Kushughulikia Ukatili wa Kijinsia katika Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati nchini , kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Novemba 25, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamisi na kulia ni Wakili Anna Meeda Kulaya ambaye ni Mratibu wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Mwongozo wa Kushughulikia Ukatili wa Kijinsia katika Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati  baada ya  kuuzindua  kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Novemba 25, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamisi na kulia ni Wakili Anna Meeda Kulaya ambaye ni Mratibu wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo


Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa Kampeni ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza katika uzinduzi huo kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, Novemba 25, 2021.
 (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.