Habari za Punde

Kamati ya Utendaji ZAPSU yakutana

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Cha Wafanyakazi wa huduma za Umma Zanzibar (ZAPSU),wakiwa katika kikao na kupitia Taarifa za Mwaka Mmoja ili kutoa mapendekezo  kwa ajili ya kupeleka Baraza kuu hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hospitali ya Maradhi ya akili Kidongo Chekundu Mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafamyakazi wa huduma za Umma Zanzibar (ZAPSU) Mwatum Khamis Othman aliyevaa mtandio (mweusi), pembeni yake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Ameir Mwadini Nahoda, wakiwa katika kikao na kupitia Taarifa za Mwaka Mmoja ili kutoa mapendekezo  kwa ajili ya kupeleka Baraza kuu, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hospitali ya Maradhi ya akili Kidongo Chekundu Mjini Zanzibar.

(PICHA NA MARYAM KIDIKO- MAELEZO)

 Na Maryam Kidiko- Maelezo.     15/01/2021.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Cha Wafanyakazi wa huduma za Umma Zanzibar (ZAPSU), wametakiwa kujadili mambo muhimu yatayokiletea chama hicho mafanikio makubwa na kupelekea kusonga mbele.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wafamyakazi wa huduma za Umma Zanzibar (ZAPSU)Ameir Mwadini Nahoda, wakati wakijadili mambo mbali mbali yanohusu chama hicho katika Kikao cha Kamati, kwa ajili ya maandalizi ya Baraza kuu, huko Ukumbi wa Hospitali ya Maradhi ya akili Kidongo Chekundu Mjini Zanzibar.

Amesema kila Mjumbe anahaki ya kuchangia hivyo wawe huru na wawazi katika kutoa michango yao bila kuvunja sheria zilizowekwa ili kufikia lengo la kikao hicho.

Nae Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa huduma za Umma Zanzibar (ZAPSU) Mwatum Khamis Othman amesema, kikao hicho kinajukumu la kupitia Taarifa za Mwaka na kutoa mapendekezo  kwa ajili ya kupeleka Baraza kuu.

Akifafanuwa zaidi amesema Taarifa hizo ni taarifa za kazi za mwaka mmoja 2021,Bajeti ya mwaka mmoja  2021, pamoja na mpango wa kazi.

Kwa upande wao Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Cha Wafamyakazi wa huduma za Umma Zanzibar (ZAPSU), wamesema kukaa pamoja na kujadili mambo mbali mbali ya chama hicho, kutasaidia kuunda mambo muhimu yanotakiwa katika chama, ili kusonga mbele na kuendelea kuwakilisha vizuri Wanachama wenzao.

Kikao cha  Kamati ya Utendaji wa Chama Cha Wafamyakazi wa huduma za Umma Zanzibar (ZAPSU), hukaa pamoja kila baada ya miezi sita na kujadili mambo mbali mbali kwa ajili ya maandalizi ya baraza kuu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.