Habari za Punde

Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Neema Lugangira Aipongeza Kamati ya Kuu ya CCM katika Mchakato wa Kumpata Mgombea Usika wa CCM.

Na.Mwandishi Wetu.Dodoma.

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) anayewakilisha Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania bara (NGOs) Neema Lugangira ameipongeza Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake mahiri, Rais Samia Suluhu katika mchakato wa kumpata Mgombea Uspika wa CCM.

Aliyasema hayo ikiwa tayari Mgombea wa CCM aliyepitishwa kuwania nafasi hiyo ya Uspika kuwa ni Dkt Tulia Ackson ambaye atapambana na wagombea wa Vyama vyengine.

Alisema hivyo kwa sababu mchakato wa kumtafuta mgombea uspika ni jambo ambalo la kitofauti lililotokea kwenye historia ya Taifa na ilikuwa imeleta sintofahamu nyingi.

Mbunge Neema Lugangira alisema lakini kwa hekima ya Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wetu Samia Suluhu Hassqn wamefanya uchambuzi kati ya wale wagombea 71 walijitokeza na wameweza kumteua Dkt Tulia aliyekuwa Naibu Spika kugombea Uspika.

Alisema jambo hilo ni kubwa sana na la kupongezwa kwa sababu kwanza limewapa imani kubwa wao kama Wabunge kuona kwamba namna gani Kamati Kuu ya CCM inathamini na kutambua uwezo wa Wabunge waliopo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Hivyo nimefarijika sana kwamba Mgombea wa nafasi ya Uspika kupitia CCM ametokea miongoni mwetu sisi Wabunge na naweza kusema Dkt Tulia nimemfahamu kutoka mwaka 2017 nilipopata bahati ya kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT kupitia Mkoa wa Kagera na kupitia Baraza hilo nikapitishwa kwa kura za kutosha katika Uchaguzi wetu nikawa Mjumbe wa Kamati ya Utekezaji UWT Taifa” Alisema

Alisema katika kipindi cha mwaka 2017 mpaka 2020 kabla hajaingia kwenye Ubunge, Dkt Tulia amekuwa mama hodari na shupavu ambaye amekuwa ni mwalimu kwao na hata pale amekuwa akiona  mtu anakitu ndani yake amekuwa mwepesi kuwa mwalimu wa kujitolea.

“Nasema ule ualimu wake na jinsi alivyo hata ukiuliza Wajumbe wa Baraza la UWT wote wanafurahia uamuzi wa Kamati Kuu kupitisha jina la Tulia kugombea Uspika” Alisema

Hata hivyo aliongezea kuwa amekuwa Mbunge kwa mara ya kwanza 2020 mpaka sasa ni kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa na muda wote Dkt Tulia amekuwa mwalimu na mwepesi kufikika na wakati wowote unaweza kutumia ujumbe akajibu na akakushauri.

Alisema pia hata wakati mwengine wanapokosea amekuwa akiwaelekeza namna ya kuchangia wanapokuwa Bungeni kwa hiyo anaimani Kiti kimepata kiongozi hodari na shupavu.

Aidha alisema hata wakati akiwa Naibu Spika akiwa ameketi kwenye Kiti ameendesha Mijadala ndani ya Bunge kwa umahiri mkubwa sana huku akitoa uhuru wa kuchangia kwa kila Mbunge.

Mbunge Neema Lugangira alisema Dkt Tulia anauwezo na Kiti cha Spika na sio mara ya kwanza CCM kuteua Mgombea wa Uspika Mwanamke walishafanya hivyo kwa Mhe Mama Anna Makinda na hiyo inadhihiridha jinsi CCM ilivyokomaa Kisasia, Kidemokrasia na Haki Sawa za Kijinsia.

“Kwa mara nyengine napenda kuwashukuru Kamati Kuu ya Halmashuri kuu ya CCM kwa kutambua umuhimu wa kuimarisha umoja na mshikamano baina yetu ndani ya Bunge kwa kitendo cha kuwarejeshea Dkt Tulia ambae ni Mbunge mwenzao. “Alisema

Alisema hiyo imewapa imani kubwa na hamasa zaidi ya yote kutokana na uwezo mkubwa na  hakuwezi kukatokea msukomsuko wa aina yote ile kwa sababu Dkt. Tulia  amekuwa Naibu Spika kwa Miaka Mitano na sasa kwa takribani Mwaka Mmoja na kidogo hivyo anajua namna kazi za Bunge zinavyoendeshwa, tulipofikia na nini kinapaswa kufuata. 

Mhe Neema Lugangira alimalizia kwa kusema Bunge litaendelea kuishauri Serikali kwa Uimara mkubwa huku akiweka wazi kuwa suala la Wabunge wenzake kumpigia kura za Kishindo Dkt. Tulia lipo wazi, watakwenda kukamilisha kazi iliyobakia maana Wabunge wote wameunga mkono na kwa kauli moja wanasema kwama Kamati Kuu ya CCM imefanya Maamuzi Sahihi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.