Habari za Punde

Timu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali yaichapa timu ya Wizara ya Utalii bao 1-0



Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akikabidhi kombe la ushindi kwa nahodha ewa timu ya  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar

Na Maulid Yussuf , Wema

Timu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeibuka kidedea baada ya kuichapa timu ya Wizara ya Utalii bao 1-0 katika mchezo wa Fainali uliochezwa jana katika viwanja vya Amani Stadium.

Mchuano huo ulikuwa ni wa aina yake ambao ulipambwa na burudani mbalimbali zikiwemo mbwa kachoka(beni) pamoja na mziki we Cool para

Goli la pekee la timu ya Wizara ya Elimu lilifungwa na mchezaji Saleh Mgeni Musa alievalia jezi nambari 18, katika dakika ya 34 kipindi cha mwanzo kabla ya mapumziko.

Mgeni rasmi katika mchuano huo Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema Wizara itaendelea kufanya Kazi ya kujenga na kuboresha miundombinu ya michezo ili kupunguza changamoto.

Akizungumza wakati wa akifunga mashindano hayo ya Mawizara, Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma amesema, uhaba wa Viwanja vya michezo ni changamoto inayopelekea kutowapa nafasi watu wote kushiriki katika michezo

Amesema mashindano hayo yanaenda Sambamba na maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar na pia utekelezaji wa sera ya Michezo ya 2018 na pia ilani ya chama Cha Mapinduzi.

" Idara ya Michezo kwa kushirikiana na Kamati Teule ya Mashindano haya mwakani tuyafanye yawe ya aina yake Ili kuleta taswira mpya ili kuondoka madhaifu yote yaliyojitokeza" alisema

Mhe Tabia amewashukuru viongozi na watendaji wa Serikali ambao wamekubali Wizara zao, Mashirika yao na Taasisi zao kushiriki katika mashindano ambapo waliluhitimisha kwa pamoja.

Amewashukuru wadhamini waliosaidia kwa njia moja kufanikisha mashindano na kuwaomba wafadhili kuendelea kusaidia mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwani kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi.

Nae Kamishna wa Michezo Zanzibar Ameir bw Makame amesema mashindano hayo yameleta mafanikio tokea kuazishwa kwake kwa kuhamasisha wafanyakazi wa Serikali kujishughulisha na Michezo kwa kufanya mazoezi, kuongeza ushirikiano, umoja na upendo ,urafik pamoja na kutekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi kwa vitendo.

Amesema katika mashindano hayo kumejitokeza baadhi ya changamoto ikiwemo baadhi ya Wizara, Taasisi, Mashirika ya Umma kuchelewa kukabidhi fomu za usajili kwa wakati,kuchezesha wachezaji wasio na sifa.

Amesema mashindano hayo yalianza tarehe 22 disemba 2021 yalipanga kushirikisha michezo mingi lakini ilifanikiwa kufanyika michezo mitatu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.