Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amuapisha Mhe. Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Ardhi Mhe. Angeline Mabula na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kumuapisha Waziri Mabula katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula mara baada ya kumuapisha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.