Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii ,Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui,akiwaaga wageni wake baada ya kumaliza mazungumzo, akiwemo Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Abdallah Alsheryani wa kwanza (kulia), huko Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
(PICHA NA MARYAM KIDIKO / HABARI MAELEZO).
Na Ali Issa Maelezo 23/2/2022
Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amesema fursa waliyopewa na Serikali ya Saudi Arabia ya kuomba msaada wa madaktari Bingwa kuja Zanzibar kutoa huduma za kidaktari wataichangamkia fursa hiyo kwani bado wanahitaji wataalamu hao.
Ameyasema hayo leo huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja wakati alipo kutana na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanazania Abdallah Alsheryani .
Amesema Zanzibar bado inahitaji madaktari bingwa katika Sekta mbalimbali za kitabibu ili kuwapa huduma wananchi,hivyo fursa ya msaada iliyotolewa na Serikali hiyo ataichangamkia na kuhakikisha madaktari hao wanaasili Zanzibar haraka iwezekenavyo.
Amesema atafanya hivyo kwani wanahitaji madaktari wataalamu ili kutatuwa changamoto ya maradhi makubwa ya kuwasafirisha wagonjwa kupeleka nje ya nchi.
Hata hivyo amesema wanashukuru kusikia kauli hiyo ya msaada na wameipokea kwa mikono miwili.
“sisi tunashukuru kusikia kauli hii na tutaichangamkia ipasavyo” alisema Waziri Mazrui.
Aidha alisema Saudi Arabia kuleta madaktari hapa Zanzibar sio marayakwaza kuja na hiyo inatokana na urafiki wao wa mdamrefu uliozoeleka katika masuala mbalimbali ya kiafya na kibinaadamu.
Nae Balozi Abdallah Alsheryani alisema fursa hiyo waliyowapa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni Zawadi kutoka kwa Mfalme Suleiman wa Saudia aliyoitoa kwa ndugu zao wa Zanzibari ili kufaidika na huduma za kimatibabu ya maradhi mbalimbali yanayo wasumbuwa.
Aidha Balozi huyo alisema Nchi yao ina madaktari bingwa wengi,hivyo ipo haja kuleta Zanzibar wataalamu kuja shirikiana na ndugu zao kwa kutoa huduma hizo ikiwemo huduma za upasuaji hasa kwa maradhi yenye gharama.
Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kudumisha udugu wao ambao ni wa mda mrefu,ambapo wataendelea kutoa misaada mengine ya kibinaadamu.
No comments:
Post a Comment