Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amefungua Rasmi Daraja la Tanzanite pamoja na Barabara ya Kuunganisha Jijini Dar es Salaam

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kabla ya kufungua rasmi Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach, katika hafla iliyofanyika eneo la Agha Khan Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa pamoja na Balozi wa Korea hapa nchini Kim Sun Pyo kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila pamoja na viongozi wengine wa Serikali

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa wakitembelea na kukagua Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam mara baada ya kulizindua rasmi leo tarehe 24 Machi 2022.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.