Habari za Punde

DKT CHAULA AKUTANA NA BENKI YA CRDB

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula akizungumza katika kikao kilichoikutanisha Wizara na Benki ya CRDB kilicholenga kuangalia namna ya kutoa huduma ya Mikopo kwa Machinga kilichofanyika Aprili 30, 2022 jijini Dodoma.

Na WMJJWM- Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amekutana na wakilishi wa Benki ya CRDB katika kikao kilicholenga kuangalia namna ya kutoa huduma ya Mikopo Maalum  kwa Machinga.

 

Dkt. Chaula ameyasema hayo  Aprili 30, 2020 alipokutana na Maafisa kutoka Benki ya CRDB katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

 

Dkt. Chaula amesema kuwa Wizara imejipanga katika kuhakikisha kuwa kundi la Machinga linaratibiwa katika utaratibu mzuri utakaowezesha kundi hilo liweze kujiendesha kibishara na kuvuka kutoka ngazi waliopo kuwa wafanyabiashara wakubwa nchini.

 

"Kwani kundi hili walizaliwa kuishia katika kundi hilo tuwawezeshe kupata mikopo itakayowasaidia kuongeza mitaji na kukua kibishara na kuwa wafanyabiashara wakubwa watakaosaidia kuchangia uchumi wa Taifa" alisema Dkt Chaula

 

Ameongeza kuwa Wizara imeimarisha mifumo mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuratibu kundi la Machinga hivyo Taasisi za kifedha zikitumika vizuri zitaweza kusaidia kundi hilo liweze kujiendesha kibishara na kukua zaidi.

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ameiomba Benki ya CRDB kuweka mazingira wezeshi kwa Makundi mbalimbali likiwemo kundi la Machinga ikiwemo robo zenye uhimilivu ziitaziwadaidia kupata mikopo ya kukuza biashara zao.

 

Naye Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Patrick Golwike akieleza vipaumbele vya Idara katika kuhakikisha kundi la Machinga linaratibiwa katika utaratibu na mifumo mizuri ameiomba Benki ya CRDB kushirikiana na Wizara katika kuliwezesha kundi la Machinga ili liweze kupata mitaji mikubwa itakayoendesha biashara zao zaidi.

 

Akieleza namna Benki ya CRDB inavyolisaidia kundi la Machinga Mkuu wa Idara ya Wateja Mmojammoja Stephen Adili alisema Benki hiyo imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo mikopo inayoweza kutolewa kwa Makundi Maalum ikiwemo Machinga hivyo wamejipanga kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuliwezesha kundi la Machinga nchini.

 

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum yenye dhamana ya kulisimamia kundi la Machinga imeweka mipango na mikakati katika kuhakikisha kundi hilo linapata fursa mbalimbali ziwemo mikopo kwaajili ya mitaji na masoko ya bidhaa zao.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.