Habari za Punde

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Azungumza na Kamati ya Siasa ya Mkoa.Alipotembelea Ofisi ya CCM ya Mkoa huo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora.Ndg.Hassan Wakasuvi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi  Shaka Hamdu Shaka na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Buriani alipowasili Ofisi Za CCM Mkoa wa Tabora, leo asubuhi, Mei 18 , 2022.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake katika mkoa huo. 
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwa Mkoani Tabora kwa ziara ya Kikazi. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan leo Jumatano tarehe 18 Mei, 2022 ametembelea ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Ndg Hassan Mwakasubi akimkaribisha Ndg Samia Suluhu Hassan alimueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi mkoani Tabora na wananchi kwa ujumla wanaridhishwa na utendaji wa serikali anayoiongoza katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

"Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora. Haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali, tunakushukuru sana na tunakukaribisha Tabora." alisema  Ndugu Mwakasubi.

Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza tarehe 17 Mei, 2022 na ataihitimisha tarehe 19 Mei, 2022 kwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Ndg.Shaka Hamdu Shaka

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa

Itikadi na uenezi

18 Mei, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.