Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika Mdahalo pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi nyingine kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika Mdahalo pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi nyingine kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kujadili fursa mbalimbali pamoja na changamoto zinazolikabili Bara la Afrika. Mkutano huo wa 57 wa AfDB unafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo pamoja na Makamu wa Rais wa Ivory Coast Mhe. Tiémoko Meyliet Koné.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina pamoja viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja mara baada ya  ufunguzi wa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022.
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.