Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba akifungua semina kwa benki ya Maafisa waandamizi wa BancABC yenye lengo la kuwapa uelewa kuhusu Sekta ya Madini ili waweze kuwa sehemu ya sekta hiyo leo Jijini Dodoma
Mkuu wa Idara ya Mikopo wa BancABC Salehe Ramadhani akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa semina iliyotolewa na Tume ya Madini kwa maafisa wandamizi wa BancABC leo Jijini Dodoma.
Maafisa waandamizi wa BancABC wakifuatilia hotuba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba wakati akifungua semina iliyotolewa na Tume ya Madini kwa maafisa wandamizi wa BancABC leo Jijini Dodoma
Maafisa Waandamizi wa BancABC wakifuatilia hotuba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba wakati akifungua semina iliyotolewa na Tume ya Madini kwa maafisa wandamizi wa BancABC leo tarehe 17 Mei 2022 Jijini Dodoma
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amefungua semina kwa benki ya BancABC yenye lengo la kuwapa uelewa kuhusu Sekta ya Madini ili waweze kuwa sehemu ya sekta hiyo.
Mhandisi Samamba amefungua semina hiyo iliyofanyika jijini Dodoma leo Mei 17, 2022 ambayo imeshirikisha watendaji kutoka Tume ya Madini na Benki ya BancAB
“Kikubwa katika semina yetu ya leo tumeongelea kuhusu masuala ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini (local content), tunafahamu mabadiliko ya sheria ya mwaka 2010 yenye lengo la kuhakikisha kwamba watanzania wanapata nafasi ya kuendeleza Sekta ya Madini” amesema Mhandisi Samamba
Aidha, amesema kuwa Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa wawekezaji kwenye Sekta ya Madini wanaweza kupata mikopo nchini kupitia mabenki.
Amefafanua kuwa, kwa kuwapa uelewa mabenki kama BancABC inakuwa ni rahisi kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa wa madini huku wakiwa na matumaini kwamba fedha zao zinaweza kurudi kwa kuwa wanakuwa wameujua mnyororo mzima wa Sekta ya Madini.
Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa mabenki nchini kujipanga katika kupokea wawekezaji mbalimbali wakiwemo watakaokuja kuwekeza katika Sekta ya Madini ikiwa ni matokeo ya Royal tour ambayo ameifanya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mikopo wa BancABC Salehe Ramadhani amesema kuwa wamejumuika na Tume ya Madini ili kupata mafunzo ili waweze kushiriki katika kutoa mikopo kwa wachimbaji wa madini nchini.
“Tunaishukuru Tume ya Madini kwa Mafunzo haya kwani yatakuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa mikopo tumeweza kufahamu yote yanayotakiwa kufanyika ikiwemo Sheria za Madini pamoja na Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini” amesema Ramadhani.
No comments:
Post a Comment