Habari za Punde

Waziri Mkuu kuzindua Mpango Kabambe wa Uhifadhi wa Mazingira

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, 2022 akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip isdor Mpango.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa kwa vyombo vya habari leo tarehe 27 Mei, 2022 jijini Dodoma.

Alisema kuwa Mpango huo umebainisha changamoto za mazingira kuanzia ngazi ya mamlaka za Serikali za Mitaa, Mikoa pamoja na mifumo-ikolojia mahsusi nchini. Alifafanua kuwa mpango kabambe huo umetoa mapendekezo ya hatua za kukabiliana na changamoto husika kuendana na mahitaji ya kila eneo.

Aidha, Waziri Jafo Kwa muktadha huo, Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira utakuwa  ndio nyenzo muhimu katika kutoa muongozo wa kuandaa na kutekeleza miradi na programu za kuhifadhi mazingira nchini,” alisema.

Mnatambua kwamba nchi yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa Mazingira  ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji, uharibifu wa Makazi ya wanyamapori na Bioanuai. Hali hii inasababishwa na matumizi yasiyo endelevu yanayochochewa  na utegemezi mkubwa wa jamii kwenye maliasili,” alisema.

Pia waziri huyo aliongeza kuwa imebainika takriban kiasi cha hekta 469,420 za misitu huharibiwa kila mwaka na utupaji holela wa taka pamoja na uwepo wa athari za mabadiliko ya tabianchi yamekuwa ni changamoto kubwa katika nchi yetu hali inayoathiri maisha ya viumbe mbalimbali ikiwemo ya mifumo ikolojia ambapo  hadi sasa imeliletea Taifa hasara ya  takriban asilimia tano 5 ya Pato la Taifa.

Alitoa wito kuwa maadhimisho ya Siku ya Mazingira yaendelee kuwa chachu ya  kuongeza  kasi ya uhamasishaji  wa jamii  kushiriki shughuli za kuhifadhi na kutunza mazingira nchini.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Kitaifa mwaka huu yatafanyika katika hapa Jiji la Dodoma na kaulimbiu ya kitaifa inayoongoza maadhimisho haya ni ”Tanzania ni moja tu: Tutunze Mazingira” ambayo inatuhamasisha kwa pamoja kila mmoja katika shughuli zake za kila siku kutunza mazingira ya nchi yetu ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa mahali salama pa kuishi kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.