Muonekano wa Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja likiwa na madarasa 42, lililofunguliwa na Makanu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi, kiwa ni shamrashamra za Maadhidhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi akikata utepe kuifungua Skuli ya Sekondari Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, ikiwa ni Shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, wakat wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa ni Shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi akiondoa pazia na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Khadija Salum Ali, akiweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali,wakati wa Shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi akioma kitabu wakati akitembelea Maktaba ya vitabu ya Skuli ya Sekondari Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni Samrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Fukuchani wakitowa burudani wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdulla Said akitowa maelezo ya Kitaalamu ya ujenzi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja , iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Makunduchi ambae pia ni Naibu Waziri wa Elimu Tanzania Mhe.Wani Hafidh Ameir, akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe.Mhandisi Hamad Yussuf Masauni,, akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Khadija Salum Ali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi, kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi Unguja.


























0 Comments