Habari za Punde

Makabidhiano ya Ripoti ya Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa.

Mwenyekiti wa Kamati ya kizazi chenye usawa Mhe Anjela Kairuki  akimkabidhi Ripoti ya Jukwaa la kizazi chenye usawa (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, wakati wa hafla hiyo makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma ameitaka Kamati ya Kizazi chenye usawa kuwa na mashirikiano ya karibu na Wizara zinazoshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake ili kuweza kutimiza ahadi zilizowekwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ripoti ya Jukwaa la kizazi chenye usawa katika ukumbi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dodoma, amesema ili kuweza kutekeleza kiufanisi ripoti ambayo baadae italazimika kuwasilishwa kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni vyema kuwepo mashikiano kutoka pande zote mbili za Muungano.

Aidha Mhe Waziri Pembe ameipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri walioifanya hadi kufikia hatua ya kukabidhi ripoti kwa Mawaziri wanaohusika katika  ahadi hizo.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima ameitaka kamati hiyo kuipitia kwa uangalifu zaidi ripoti hiyo kabla ya kuwasilishwa kwa Mhe Rais kwani ndio ngazi ya mwisho kwa upande wa Tanzania kabla ya kuwasilishwa katika kikao cha mwezi Septemba nchini Ufaransa.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya kizazi chenye usawa Mhe Anjela Kairuki amewashukuru Mawaziri wote pamoja na watendaji wa pande zote kwa mashirikiano makubwa waliyowapatia katika kuaanda na kuipitia ripoti hiyo hadi kufikia hatua ya mwisho ya kuwakabidhi hatimae kumkabidhi Mhe Rais kwa hatua stahiki.

Kamati ya kizazi chenye usawa imekabidhi ripoti ya ahadi 11 za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimebeba  hali ya usawa wa kiuchumi kwa mwanamke.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.