Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Kamati ya Ushauri ya Kitaifa "Generation Equality Forum"

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu”Generation Equality Forum, ukiongiozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Angela Kariuki (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 15-6-2022, walipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu “Generation Equality Forum” Mhe. Angela Kariuki, akitowa maelezo ya Kazi ya Kamati hiyo wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,akiwa na Ujumbe wake walipofika kujitambulisha leo 15-6-2022, (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mgeni Hassan Juma.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu”Generation Equality Forum, ukiongiozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Angela Kariuki (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 15-6-2022, walipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu “Generation Equality Forum” baada ya kumaliza mazungumzo yao walipofika Ikulu Zanzibar leo. Angela Kariuki15-6-2022.(Picha na Ikulu)

Rais Dk. Mwinyi alikutana na Kamati ya Kitaifa ya Ushauri ya Utekelezaji wa Ahadi za Nchi za Kizazi chenye Usawa (GEF), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki ambapo ameihakikishia Kamati hiyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaufikisha Mpango wa Utekelezaji wa Kamati hiyo katika Baraza la Mapinduzi ili Serikali nzima iuelewe kwa undani zaidi na kuufanyia kazi.                                                                                

Alieleza kufurahishwa na utaratibu wa kupata matokeo yanayotarajiwa kwani ni njia nzuri ya kupata matokeo yanayotarajiwa na pia,  ni njia nzuri za kufanya tathmini.

Aliupongeza Mpango wa Kamati hiyo kwa kujikita na mambo muhimu na kueleza kwamba juhudi za makusudi zitafanyika katika kuhakikisha bajeti maalum inawekwa kwa Wizara husika ili kufanikisha Mpango huo.

Mapema, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Angellah Kairuki alitumia fursa hiyo kuitambulisha Kamati pamoja na kumjuulisha Rais jitihada zilizofanyika tangu kuzinduliwa rasmi kwa Kamati hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Disemba 16, 2021 huko Jijini Dodoma. 

Alisema kuwa katika kuhakikisha utekelezaji wa ahadi za nchi, Kamati hiyo ya Ushauri ya Kitaifa yenye wajumbe 25 kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu ya Juu, Taasisi za Utafiti na Sekta binafsi ambapo wajumbe 19 kutoka Tanzania Bara na 6 kutoka Zanzibar imeundwa ili kushauri jinsi ya kuhakikisha ahadi za nchi zinafikiwa.

Mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kuunda Wizara inayojitegemea inayoshughulikia masuala ya Jinsia, Wazee na Watoto kwani ni chombo muhimu sana katika haki na usawa wa kiuchumi kwa wanawake.

Aidha, alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kuendelea kuwa kinara na mhamasishaji wa kampeni ya He for She’ ambayo ni mkakati muhimu sana katika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake.

Sambamba na hayo, Mwenyekiti Kairuki alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kwamba Kamati hiyo iko tayari kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuhakikisha inapata matokeo tarajiwa.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano,

Ikulu Zanzibar. OF RESPONSIBILITY

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.