Habari za Punde

Miaka Minane ya Mwanzo na Makuzi ya Mtoto.

Na MJJWM, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amewataka waandishi wa habari kuelemisha jamii kuhusu Programu ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto na umuhimu wa kutoa Malezi Bora ndani ya kipindi cha Umri miaka 0 hadi 8.

Dkt.  Gwajima ameyasema hayo jijini Dodoma Julai 4, 2022 wakati akifungua Mafunzo ya Kitaifa ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ambapo jumla ya Washiriki 79 kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanapatiwa Mafunzo ya siku sita.

Dkt. Gwajima amesema kuwa kwakuwa Mafunzo hayo yanawashirikisha na watu wa Kada zingine  ambao ni Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii lakini pia kutoka Asasi za kiraia ni imani yake kuwa tija iliyokusudiwa itapatikana wakishirikiana.

Ameongeza kuwa Waaandishi wa Habari ni kada muhimu sana katika kusukuma Ajenda za Maendeleo ya Makuzi na Maendeleo ya Mtoto, hivyo wakitumia  kalamu zao vizuri wataweza kuinua taaluma zao lakini watasomeke vema kwa Taifa kwa uzalendo wao.

"Lingine lakufurahisha ni kuwa Mafunzo haya yamehusisha pande hizi mbili za Muungano lakini ifahamike mwingiliano wetu na kutembeleana Mara kwa Mara kati ya pande mbili hizi itachochea na kuimarisha zaidi Muungano wetu, kitu ambacho hata Rais  Mhe Samia Suluhu Hassan  amekuwa akikisisitiza" amesema Waziri Gwajima.

Kwa Upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum ambaye ni Mkurugenzi wa Watoto, Sebastian Kitiku alisema Elimu kwa Kada hizo ni Mwanzo wa kuzifikia kada zingine ili ziweze kushiriki kawamakribu katika kuhakikisha jamii inapata uelewe wa namna ya kuwaoatoa Watoto malezi bora kupitia Programu hiyo

"Mhe. Waziri Elimu hii ambayo inatolewa kwa muda wa siku sita ni mwanzo tu lakini Shabaha yetu nikuwafikia watu wa Kada zote nchi nzima kwakuwatumia Maafisa Ustawi na Maendeleo ambao wamepata elimu hii" alisema Kitiku.

Akitoa Maelezo kuhusu Mafunzo hayo Mkurugenzi Mkaazi Craig Ferla  kutoka taasisi ya Crossfire alisema muelekeo ni kuandaa Kadi ya kujipima kwa kila mmoja ili kuona kama wanapiga hatua kutokana na elimu inayotolewa na lengo likilokusudiwa.

"Mhe. Waziri utakumbuka ulipo muwakilisha Mhe. Rais wakati wa uzinduzi wa Program hii uliagiza suala la Score Card leo tunaomba tukuhakikishie kuwa suala lile tumelizingatia hivyo katika utendaji wetu tumeona tuwe nalo" alisema Craig.

Washiriki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakiwepo Maafisa waandamizi kutoka Serikali kuu, Mikoa na kutoka Asasi za Kiraia wakiwepo Waandishi wa Habari vinara kutokea Klabu za Waandishi wa Habari wanashiriki mafunzo ya siku sita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.