Habari za Punde

Hospitali ya Kisasa Kujengwa Fumba Mwaka Huu

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na Ujenzi wa Hospitali ya kisasa unaotarajiwa kuanza Novemba chini ya ufadhili wa Alfalasi Foundation huko Fumba  Wilaya ya Magharibi "B " ,hafla iliyofanyika Ukumbi wa  Verde Mtoni Zanzibar

Mkuu wa Alfalasi Foundation Ahmad Alfalasi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Ujenzi wa Hospitali ya kisasa unaotarajiwa kuanza Novemba chini ya ufadhili wa Alfalasi Foundation huko Fumba Wilaya ya Magharibi B ,hafla iliyofanyika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 


PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR                      


Na Ali Issa Maelezo 02/08/2022.

Taasisi ya Al falasi Foundation kutokaumoja wa Falme za Kiarabu UAE inatarajia kutoa vifaa vya msaaada vya uchunguzi wa maradhi ya binaadamu katika hospitali ya Abdalla Mzee kusini Pemba.

Akizungumza na waandishi wa habari huko mtoni katika Hotel ya Verde, Mfadhili Mkuu wa Taasisihiyo Ahmad AlFalasi alisema vifaa hivyo ni mashine za uchunguzi wa maradhi ya Figo, maradhi ya Homa ya Ini, Saratani, pamoja Vitanda 600vya kulaza wagonjwa na magodoro yake pamoja na vifaa vya maradhi mengine yanayowasumbuwa binaadamu.

Alisema msaada huo anautoa kwa ndugu zao wa Zanzibar ili wafaidike kupata huduma za matibabu ya maradhi kwa uhakika.

Aidha alisema kuwa Taasisi yake   inakusudia kujenga Hospitali kubwa yenye vifaa vya kisasa katika eneo la Fumba.

Aidha alisema tayari washazungumza na watu wa ZIPA na washapati wa mkataba rasmi wa kuanza kazi hiyo na matarajio yao ujenzi huo utamaliza kwakipindi cha mwaka mmoja.

Nae Waziri  wa Afya Nassor Ahmed Mazrui alisema wanaishukuru Taasisi hiyo kwa misaada yake wanayoitoa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Z anzibar na kusema Taasisi hiyo inamoyo wa  imani kwa kuisadia  Zanzibar  katika suala zima la matibabu ya maradhi mbalimbali ikiwemo maradhi yasioambukiza na mengineyo .

Hata hivyo alisema kuwa serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar itatoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ili kufanikisha azma waliokusudia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.