Habari za Punde

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan afunga Mafunzo ya Awali ya Askari wa Uhamiaji kozi Na.1/2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Cheti kwa Mshindi wa Jumla kwenye Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji Konstebo Geofrey Felician Zakaria, wakati wa Ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyoshirikisha jumla ya Wahitimu 818 katika Chuo cha Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Jeshi la Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipanda mti mbele ya Jengo la Ofisi za Chuo cha  Jeshi la Uhamiaji  Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, alipowasili Chuoni hapo kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari 820 wa Jeshi la Uhamiaji tarehe 15 Agosti, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Salaam na Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Jeshi la Uhamiaji  Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji tarehe 15 Agosti, 2022.

 

Askari wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Uhamiaji Kozi Na. 1,2022 wakila kiapo cha Utii mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwenye Hafla ya ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kabla ya kufungua Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji katika Hafla iliyofanyika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Askari wahitimu wa Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji pamoja na Wananchi katika Hafla ya Ufungaji wa Mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.