Habari za Punde

Mwakilishi wa Chama cha Wasioona Sweden (SRF) wakutana na Chama Cha Wasioona Zanzibar (ZANAB)

Mwakilishi wa  Chama cha Wasioona Sweden (SRF)  Bi Eva Nilson akizungumza wakati walipokutana na Chama Cha Wasioona Zanzibar (ZANAB) kujadili Maendeleo ya  Mradi wa kuwarejesha watoto Wasioona na wenye ulemavu wa ngozi  mashuleni unaofadhiliwa na SRF na kutekelezwa katika  Wilaya ya Wete, Kaskazini "A" na Wialaya  ya Kati Unguja ,hafla iliyofanyika  Ofisi ya ZANAB Kikwajuni Weles Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Zanzibar  (ZANAB) Fatma Djaa Chess akizungumza wakati wa hafla ya majadiliano kuhusiana na Mradi wa kuwarejesha watoto Wasioona na wenye ulemavu wa ngozi  mashuleni unaotekelezwa na Chama Cha Wasioona Sweden (SRF) katika Wilaya ya Wete, Kaskazini "A" na Wilaya ya Kati Unguja,huko Ofisi za ZANAB Kikwajuni Zanzibar. 
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Daily News Issa Yussuf akimuuliza baadhi ya maswali kuhusiana na watu wasiona Mwakilishi wa  Chama cha Wasioona Sweden (SRF)  Bi Eva Nilson wakati wa majadiliano kuhusu mradi wa kuwarejesha watoto Wasioona na wenye ulemavu wa ngozi mashuleni, huko Ofisi za ZANAB Kikwajuni Zanzibar.

Wajumbe Chama cha Wasioona Zanzibar (ZANAB) wakiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Wasioona Sweden (SRF).

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.