Habari za Punde

Shaka Aishukuru TARURA Kuvunja Mikataba na Wakandarasi Wababaishaji

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka Amemshauri Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za  Vijijini  na Mijini  (TARURA), Mhandisi Victor Seff kuwasimia vyema mameneja wa TARURA wilaya na mikoa ili kuhakikisha wakandarasi wababaishaji na walioonesha uwezo mdogo kwenye utekelezaji wa miradi ya barabara wanasitishiwa mikataba na kutokupewa kazi za TARURA nchi nzima.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa kata ya Igulungu, Jimbo la Tabora Kaskazini baada ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari Gilimba katika Halmashauri ya Wilaya  ya Uyui Mkoani Tabora ambayo ipo katika hatua ya ukamilishaji.

Shaka aliyasema hayo baada ya wananchi kulalamikia ubovu wa barabara yao ya Igulungu ambayo ina mkandarasi anayeijenga na amelipwa kiasi cha shilingi milioni 60 kati ya shilingi milioni 499 za mradi huo lakini kazi inasuasua na hata maeneo aliyoyajenga ipo chini ya kiwango. 

Shaka amesisitiza kuwa lengo la kuanzishwa kwa TARURA nchini ni kuhakikisha  inawasaidia wananchi katika Suala zima la ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwarahisisha katika usafirishaji wa mazao, bidhaa na kwenye kufuata huduma za kijamii.  Hivyo  ni muhimu kutumia wakandarasi  wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi ili kuhakikisha miradi wanayopatiwa na Serikali inakamilika kwa wakati. 

Wakati Huo huo Chama Cha Mapinduzi kimeahidi kukutana na Baraza la uwezeshaji wa  Wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa lengo la kuweka mipango thabiti itakayowezeshwa vijana kufikiwa na fursa zilizopo nchini ikiwa hatua mojawpao ya kukabiliana na changomoto ya ajira.

Shaka ameeleza hayo  baada ya kufanya ziara ya kutembelea SIDO Mkoa wa Tabora ambapo amesema kumekuwepo na  mifuko mingi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi wakiwemo vijana lakini ukishuka chini kabisa vijana bado hawafahamu fursa zilizopo.

Shaka amesema  bado tatizo la ajira kwa vijana inaonekana ni kubwa lakini tayari Serikali imeweka jitihada kubwa kwenye eneo hilo na Ilani ya Uchaguzi ibara ya 83 imeagiza na imeelekeza ndani ya kipindi cha miaka mitano watakwenda kuzalisha ajira zaidi ya milioni saba kupitia taasisi za umma na taasisi ambazo sio rasmi.

Muuzaji wa nyama ya kuchoma Bi Annastazia  akifurahia baada ya  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, Kutembelea Mnada wa Igunga akiwa ziarani mkoani Tabora


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wana CCM katika jimbo la Manonga Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora, baada ya kukagua Shule ya Sekondari Kitangiri, akiwa katika ziara mkoani Tabora
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wana CCM katika jimbo la Manonga Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora, baada ya kukagua Shule ya Sekondari Kitangiri, akiwa katika ziara mkoani Tabora,  
(Picha na Fahad SIRAJI wa CCM).
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.