Habari za Punde

Tamasha la Kizimkazi CRDB Bank Ngalawa Race Lafana Mkoa wa Kusini Unguja

Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma (watatu kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili na nusu (2,500,000/-), Khatib Haji Hamis (wapili kushoto) aliyeibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, yaliyofanyika leo Agosti 30, 2022 kwenye fukwe za Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid, Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Rajab Yussuf Mkasaba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Insurance Broker LTD, Wilson Mnzava.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, yaliyofanyika  Agosti 30, 2022 kwenye fukwe za Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, yaliyofanyika  Agosti 30, 2022 kwenye fukwe za Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Sehemu ya wananchi wakiendelea kufurahia burudani mbalimbali katika mashindano ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, yaliyofanyika  Agosti 30, 2022 kwenye fukwe za Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Elias Barnabas maarufu kama Barnaba akitoa burudani wakati wa mashindano ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, yaliyofanyika  Agosti 30, 2022 kwenye fukwe za Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.