Habari za Punde

Wazazi waaswa kuwapatia watoto chanjo ya Polio

  Na Khadija  Khamis  Maelezo.  


Afisa wa Afya Wilaya ya Mjini , Faki Makame Faki amewataka wazazi na walezi kutoa mashirikiano ya kuwapatia chanjo ya polia watoto wao ili kupata kinga ya maradhi hayo.


Akitoa wito huo katika Ukumbi wa Wilaya ya Mjini , Sebleni wakati akitoa taarifa ya Kampeni ya Chanjo inayoendelea katika wilaya hiyo kwa Waandishi wa habari .


Amesema ufahamu mdogo kwa wazazi na walezi hupelekea kuwakosesha haki ya msingi ya kupatiwa chanjo watoto wao hivyo kusababisha kupata ugonjwa huo hatari wa Polio .


Akizungumzia dalili za ugonjwa huo alisema ni kuwa na homa kali sana na kupata ulemavu wa ghafla wa viungo vya mguu na mkono.


Aidha alisema ugonjwa huo unasababishwa na virus aitwae (Polio Virus) ambae hushambulia mifumo ya mmen’genyu wa chakula mwilini  na kupeleka kutapika na kuharisha .


Alifahamisha kinga yake ni kukosha mikono kabla na baada ya kula, pindi unapotoka chooni na kuweka mazingira yanayokuzunguka katika hali ya usafi .


Nae  Mratibu wa Elimu ya Afya Wilaya ya Mjini, Risk Mohamed Suleiman  amasema zaidi  ya watoto  47,698, wamepatiwa chanjo katika kampeni hiyo wenye umri wa chini ya miaka mitano .


Alifahamisha kuwa mnamo Febuari 2022 nchini maiawi kulitokea mripuko wa maradhi hayo hivyo Shirika la Afya Ulimwenguni  (WHO) imezitaka nchi zote za jirani  kupatiwa chanjo hiyo .


Alieleza tangu Julai 1996 hakuna mgonjwa alieripotiwa kwa nchini Tanzania hadi 2015, kupata tunzo kwa kuyathibiti maradhi hayo .


Kampeni ya Chanjo ya Polio itaanzia  Septemba 1 hadi 4  kwa awamu hii na zoezi hilo litahusisha nyumba kwa nyumba kwa kushirikiana na timu ya uhamasishaji . 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.