Habari za Punde

Tunathamini na Kutambua Mchango wa India : Balozi Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula Balozi Mulamula akizungumza wakati wa hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Amin Juma Mohamed akizungumza wakati wa hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamaica Mhe.  Kamina Jonhson Smith akizungumza wakati wa hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula Balozi Mulamula akiwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali  katika hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.
Baadhi ya washiriki wa  hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema Tanzania inathamini na kutambua mchango mkubwa wa India katika kuendeleza miradi ya maji na afya nchini na hivyo kusaidia jiotihada za Tanzania katika kutekeleza malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa na dira ya Tanzania ya Mwaka 2025 .

Balozi Mulamula ametoa kauli hiyo katika hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.

 

“TANZANIA inathamini na kutambua mchango wa India katika kuisaida serikali kutekeleza mipango yake ya maendeleo, na tunaamini kuwa ushirikiano uliopo utakuwa zaidi na zaidi kwani ushirikiano huo ni matunda ya uhusiano wa nchi za kusini na kusini,”

 

Amesema uhusiano na Indi unachangia juhudi za Tanzania kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Afya na ustawi wa watu na maji safi na salama na hivyo kuchangia utekelezaji wa dira ya Tanzania ya mwaka 2025 na kuongeza kuwa ni mmoja ya wawekezaji wakubwa nchini ambaye anachangia asilimia 16 ya biashara ya Tanzania na kuchagiza utekelezaji wa dira yetu ya 2025.

 

Ametaja miradi inayonufaika na ushirikiano huo kuwa ni usambaza maji Dar es Salaam hadi Chalinze wenye thamani ya Dolla za Marekani Milioni 178 ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu. 

Miradi mingine ni usambazaji wa bomba la maji kutoka Ziwa Victoria hadi  Tabora, Igunga, na Nzega uliozinduliwa mwezi January 2021; kusambaza bomba la maji kwenda katika miji ya Tinde na Shelui na vijiji vya jirani wenye thamani ya dola milioni 10.64 za Marekani ambao unaotarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2022; na mradi wa ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika miji 28 Tanzanian wenye thamani ya dola milioni 500 za Marekani ambao utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwezi Disemba 2022.
 

Kuhusu sekta ya Afya Balozi Mulamula amesema Tanzania inaishukuru India kwa mchango wake kwa Tanzania kujiweka tayari kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 hasa kwa kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya afya, kuongeza nguvu ya watumishi wa afya nchini na kuongeza uwezo wa nchi kutengenza dawa, ugavi, chanjo na vifaa tiba.
 

Tarehe 15 Agosti 2022 India  iliadhimisha miaka 75 ya kuwa Jamhuri na miaka 76 tangu ipate uhuru  kuadhimisha miaka 75

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.