Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Luteni Kanali Selestine Masalamadu akifungua warsha ya Uchambuzi wa Gharama na Manufaa ya Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja nchini iliyofanyika Jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu-Dodoma
Kikao cha Uchambuzi wa Gharama na Manufaa ya Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja nchini ambayo lengo lake ni kukabiliana na magonjwa yanayowakumba bindamu, wanyama na mimea.
Kikao hicho kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 8 hadi 9 mwaka huu kilifunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Luteni Kanali Selestine Masalamadu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Aidha kinalenga kufanya uchambuzi huo ili kuonesha thamani yake na kuvutia uwekezaji wa rasilimali kutoka kwa serikali na wadau mbalimbali wa afya moja.
Mshauri kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Dkt. Janeth George (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya Uchambuzi wa Gharama na Manufaa ya Utekelezaji wa Afya Moja nchini.
No comments:
Post a Comment