WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Kassim Majaliwa akitowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Mtoto wa Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, alipofika nyumbani kwa marehemu Chukwani Wilaya ya Magharibi "B"Unguja leo 2-9-2022, kwa ajili ya kutowa mkono wa pole..(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakipokea mkono wa pole kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Kassim Majaliwa, alipofika nyumbani kwa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kutowa mkono wa pole kwa Familia ya marehemu leo 2-9-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Kassim Majaliwa wakiitikia dua ya kumuombea Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi ,ikisowa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, baada kutowa mkono wa Pole kwa Familia ya marehemu nyumbani kwake chukwani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 2-9-2022.(Picha na Ikulu)
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 02 Septemb
WAZIRI Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim
Majaliwa leo ameifariji Familia ya Rais
Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi
kutokana na kifo cha mtoto wake Hassan Ali Hassan kilichotokea Jumatano wiki hii katika
Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Hafla hiyo ilioambatana na Dua ilifanyika nyumbani
kwa Marehemu Chukwani Mkoa Mjini Magharibi ambapo Waziri Mkuu pia alipata fursa
ya kutoa mkono wa pole kwa Rais mstaafu
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mama Siti Mwinyi, Mke
wa marehemu Fauzia Salim Hilali pamoja na wanafamilia.
Waziri Mkuu Majaliwa alimuomba
Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake marehemu, huku akiwataka wafiwa kuwa na
moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wao.
Imetayarishwa
na Idaya
No comments:
Post a Comment