Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Aendelea na Ziara Yake Nchini Oman Atembelea Bandari ya Sohar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi katika Muendelezo wa ziara yake leo ni siku ya tatu ya tarehe: 13 Oktoba 2022 ambapo ametembelea Eneo la Bandari ya Sohar na  maeneo huru ambayo yanajumuisha maghala ya Chakula, mali ghafi za kutengeneza vyuma  na viwanda katika eneo hilo.

Miongoni mwa viwanda vilivyomo ndani ya eneo hilo la Bandari ya Sohar ni pamoja na kiwanda cha utengenezaji wa vyuma, mbolea, dawa, sukari, pia huagiza mali ghafi kutoka nchi mbalimbali Duniani. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika eneo la Bandari ya Sohar  Nchini Omar wakati wa ziara yake Nchini humo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika eneo la Bandari ya Sohar  Nchini Omar wakati wa ziara yake Nchini humo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea eneo la Bandari ya Sohar Nchini Oman akiwa katika ziara yake Nchini humo, akipata maelezo kutoka kwa mwenyeji wake shighuli zinazotolewa na Bandari hiyo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha wageni wakati wa ziara yake kutembelea Bandari ya Sohar  Nchini Omar wakati wa ziara yake Nchini humo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Kiongozi wa bandari ya Sohar Nchini Oman akitowa maelezo ya michoro ya majengo yaliyoko katika bandari hiyo, wakati wa ziara yake kutembelea bandari hiyo kujionea shughuli zinazotolewa na bandari hiyo hupokea na kusafirika mizogo mbalimbali. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.