Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema Utafiti wa
Viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania ni muhimu kwani utawezesha Serikali
na Wadau tofauti kupata hali halisi ya mwenendo wa maradhi hayo na kusaidia
kuweka mikakati ya kwenda sambamba na uhalisia katika kupambana na tatizo hilo.
Mhe. Othman
ameyasema hayo huko hotel ya Verde Mtoni wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini
Maghari alipozungumza katika uzinduzi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya
Ukimwi nchi utakaofanyika Tanzania Bara na Zanzibar.
Amefahamisha
kwamba kupatikana kwa takwimu sahihi ni silaha muhimu katika kupanga na
kuaandaa mikakati ya kupambana na
maradhi hayo kwa kuwa itasaidia kufahamika mwendendo wa tatizo hilo kwa
ukamilifu kote nchini.
Hata hivyo,
Mhe. Othman amesema kwamba kwa upande wa Zanzibar ni vyema utafiti huo kwenda
sambamba na utafiti wa viashiria vya
Maambukizo ya Virusi vya Ukimwi kwa kuhusisha makundi maalum ambayo
yanaaminiwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya maradhi hayo
ikilinganishwa na jamii ya kwaida.
Amefahamisha
kwamba utafiti huo utahusisha Kaya zipatazo 20 alfu kwa Tanzania Bara na Zanzibart na kuwataka wananchi kuondoa hofu juya suala
hilo na kuwataka kuona kwamba kaya zote zina fursa sawa ya kushiriki kwenye utafiti huo.
Mhe. Makamu
amesema kwamba kwa ujumla inatarajiwa kwamba utafiti huo utahusisha watu wapato
40 alfu kushiriki kwa utafiti wa mwaka
2022/2023 na kwamba ni matumaini ya serikali kwamba kaya zilizochaguliwa na watu watakaohusika watatoa ushirikiano wa
kutosha katika kufanikisha suala hilo muhimu na kwamba taarifa zitakazopatikana
zitaendelea kuwa siri na zitatumika kitakwimu pekee.
Amesema
kwamba Tanzanzia inayo mikakati kadhaa ya kupambamba na tatizo hilo kwa kuwa ni
muhimu pia katika kusaidia nchi kupiga hatua kiuchumi kuwa kuwepo jitihada na
mikakati imara ili wananchi waepukane na maradhi ikiwemo janga la Ukimwi.
Mhe. Othman
amezishukuru serikali ya Marekani kupitia kituo chake cha Kudhibiti na kuzuia
Magonjwa kwa kuendelea kuisaidia nchi
Kitaalamu na Kifedha kuweza kufanya
utafiti huo muhimu katika kupambana na maradhi ya Ukimwi.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Dk. Ahmed Khatib, amesema kwamba
Zanzibar kumekuwa na mkikakati mbali mbali mbali ambayo imesaidia sana katika
kupambana na kudhibiti janga hiloi tokea ilipobainika mgonjwa wa kwanza mwaka
1986 hapa Zanzibar.
Naye
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndugu Salim Kassim Ali,
asmesema kwamba utafiti huo utawahusisha watu kuanzia umari wa miaka 15 na
kuendelea na kwamba takwimu
zitakazopatikana zitasaidia sana katika kubuni sera mpya na kupanga mikakati
zaidi ya kupambana na janga hilo.
Utafiti huo unasimamiwa kwa pamoja kati ya Tume ya
Ukimwi Zanzibar na Tanzania Bara, Ofisi za Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar na
Tanzania Bara pamoja na mashirika mbali mbali ya kimataifa ikiwemo Marekani,
Who na mengineyo.
No comments:
Post a Comment