Habari za Punde

CCM yateua mgombea wa Jimbo la Amani kwenye uchaguzi mdogo

 UTEUZI WA MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM, UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA AMANI, ZANZIBAR.


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana Dodoma katika kikao chake maalum, Jumanne tarehe 22 Novemba, 2022 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine kamati  kuu imefanya uteuzi wa mgombea wa nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Amani Mjini Zanzibar ambapo imemteua Ndugu Abdul Yusuf Maalim kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 17 Disemba, 2022.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Marehemu Mussa Hassan Mussa kilichotokea tarehe 10 Oktoba, 2022.

Aidha Kamati Kuu imepokea taarifa ya maendeleo ya uchaguzi  wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake unaoendelea katika ngazi ya mikoa nchini ambapo imeendelea kuwakumbusha wanachama, viongozi na wagombea wote juu ya umuhimu ya kuheshimu miiko ya uongozi kwa mujibu Katiba na Kanuni za chama.
 
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na Uenezi.
22 Novemba, 2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.