NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR 22/11/2022
Kamishna wa Intelijensia ya Jinai, Charles Mkumbo amefungua mkutano wa Kimataifa kuhusu kubadilishana taarifa na
uzoefu kwa uhalifu unaochupa mipaka huko Michamvi Mkoa wa Kusini Unguja
Visiwani Zanzibar .
Amesema Mkutano huo ni fursa muhimu
kwa nchi washiriki kubadilishana uzoefu katika kuzuwia na kukabiliana na
changamoto za kiusalama hasa kwa uhalifu unaovuka mipaka.
Mkutano huo wa siku tatu
umezishirikisha nchi ya Gabon, Congo DRC, Malawi, Niger, Uganda na wenyeji
Tanzania na kufadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment