Habari za Punde

Mwenyekiti wa NEC akagua zoezi la upigaji wa kura kwenye Uchaguzi Mdogo Jimbo la Amani Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 17 Disememba, 2022, ametembelea na kukagua zoezi la upigaji wa kura kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Amani Zanzibar. 


Jaji Mwambegele ameridhishwa na maandalizi ya vituo, kufunguliwa kwa vituo na ulinzi wa vituo. Vituo vimefunguliwa saa 01:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni. Uchaguzi huo unafanyika sambamba na kata saba (7) za Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.