Habari za Punde

Kikao cha Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar

Mjumbe wa kikao akitoa mchango mara baada yakujadili dodoso katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Baraza la Mwanakwerekwe Wilaya ya  Magharib “B” Mjini Zanzibar,
Mmoja kati ya wajumbe Riziki Shehe Bakar  walioshiriki katika kikao hicho  akiwasilisha mada  zilizojadiliwa katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Baraza la Mwanakwerekwe Wilaya ya  Magharib “B” Mjini Zanzibar, (kulia) Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Said Kassim Marine.

Baadhi ya wajumbe waolishiriki katika kikao cha Baraza la michezo wakiangalia dodoso zinazojaliwa katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Baraza la Mwanakwerekwe Wilaya ya  Magharib “B” Mjini Zanzibar, (kulia) Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Said Kassim Marine.

                                 Picha na Miza Othman (BTMZ).                           

Na Miza Othman- (BTMZ).  20 /01/2023.

Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar  limeona ipo haja ya  kutumia mbinu mbadala ya kuwashawishi vijana  katika kushiriki michezo mbalimbali  kwani kufanya hivyo  kutaondokana na wimbi kubwa la vijana  kujishirikisha na vikundi viovu na kutapelekea kukuza maendeleo ya Taifa  Nchini kwao.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Ndugu  Mwalim Ali Mwalim  aliyasema hayo wakati walipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza katika kikao cha kawaida cha robo ya pili  cha Baraza la Michezo kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Mwanakwerekwe Wilaya ya  Magharib “B” Unguja.

Alisema ni vyema Wajumbe wa Baraza hilo  kuwa makini katika kutekeleza majukumu ya kazi zao kwani kufanya hivyo kutasaidia  kurahisisha usimamiaji na uendelezaji wa shughuli za michezo hapa Zanzibar.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema upo muhimu wa sekta ya michezo kupewa kipaombele  kwani sekta hiyo  inasaidia  kuwanyanyua vijana kuondokana na utegemezi katika kujikwamua Maisha yao na  kulinyanua taifa kiuchumi .

“Hakuna mtu yeyote anaweza kushawishiwa kuingia ndani ya michezo kwani ni maamuzi ya mtu mwenyewe kushiriki mfano wachezaji kama Pele, Bekam kutokana hivi sasa wanapata fursa za kushiriki maamuzi ya vikao mbalimbali katika taifa”, Alisema Mwenyekiti.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Said Kassim Marine alisema Baraza la Michezo  limeona upo umuhimu wa kuanzisha tamasha la michezo litakazoweza kuwainua vijana na kuonyesha vipaji walivyonayo kwa  kuonekana ndani ya mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Hata hivyo aliwataka wajumbe hao kushiriki katika vikao mbalimbali vinavyojadiliwa na kuweza kubuni mambo yatakayowawezesha kuibuwa njia za kukuza michezo hapa nchini kwao.

 Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho walisema ni vyema  kuandaa kanuni na  sheria na kufanyiwa kazi  kwani kufanya hivyo kutapelekea kurahisisha utekelezaji wa  kazi zao kwa uhakika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.