Habari za Punde

Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ametoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Shabaan Iddi Mabrouk

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na  Wananchi na wanafamilia ya Marehemu Bw,Shaaban Iddi Mabrouk, Ndugu wa Makamo Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Bi.Dogo Iddi Mabrouk Kwahani Wilaya ya Mjini alipofika kutoa mkono wa pole
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipofika kuwapa pole familia ya Makamo Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Bi.Dogo Iddi Mabrouk aliyefiwa na kaka yake  Marehemu Bw,Shaaban Iddi Mabrouk, Kwahani Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) akiitikia dua iliyoombwa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume (kulia) mara alipofika kutoa pole kwa  Familia ya  Marehemu Bw,Shaaban Iddi Mabrouk, Ndugu wa Makamo Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Bi.Dogo Iddi Mabrouk Kwahani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
[Picha na Ikulu] 27/03/2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.