Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, akizungumza wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa Viongozi wa Serikali, Dini, Vyama vya Siasa na Watu Mashuhuri mbali mbali, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amesema kwamba ni vyema kwa Viongozi wenye
dhamana na dhima mbali mbali nchini kuyachukuwa kivitendo mafunzo ya imani na
nidhamu yanayopatikana ndani ya Mwezi mtukufu ili kuifanya Zanzibar kuepukana
na masuala mbali mbali yanayoirejesha nyuma
kwa kuamini kwamba Mwenyezi Mungu yupo wakati wote.
Mhe. Othman ameyasama hayo huko
katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul -Wakili Kikwajuni Mjini Zanzibar
alipowasalimia viongozi na wananchi mbali mbali mara baada ya kukamilika futari
ya pamoja iliyoandaliwa na ofisi yake na kujumuisha wananchi mashuhuri wakiwemo
mawaziri na viongozi mbali mbali.
Mhe. Makamu amesema kwamba mikusanyiko
ya kibaada ikiwemo futari ya pamoja
wanayokaa wananchi na waumini mbali mbali inasaidia sana kuvunja na
koondosha mambo yanayotenganisha
wananchi na kuongeza ihsani miongoni mwao ikiwa ndiko kuuthamini msingi wa kuwa pamoja
na kupata fadhala nyingi kutoka kwa mola muumba.
.Mhe Makamu amesema kwamba mikusanyiko
ya namna hiyo ni muhimu na inatoa fadhila
nyingi za mwezi mtukufu wa ramadhani na kuweza kutumia fursa ya mwezi mtukufu wa
ramadhani kwa mja kuomba msamaha kwa
aliyokosea na kuwa na uhakika wa msahaha ikiwemo kupata fadhila na darja
kubwa ukiwemo usiku mtukufu wenye kheir nyingi zaidi wa laylatul-kadri.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba ni
wajibu wa waumini kumshukuru Mola muumba na kuwakumbusha wananchi na waumini wa Kiislamu kwamba, mbali ya
fadhila za ramadhani zilizowekwa na Mola
muumba, lakini pia mwezi huo ni chuo muhimu cha elemu ya kujenga nidhamu ya
yakini kwa mwenyezimungu muumba.
Amesema kwamba suala la kujengeka
nidhamu miongoni mwa waumini na wananchi linasaidia sana taifa kupiga hatua na kupata
maendeleo na kamwe hakuna mwananchi ama
kiongozi anayeweza kufanikiwa kwa lolote bila kufuata nidhamu na kwamba mwezi mtukufu wa ramadhani unatoa
funzo kubwakwa jambo hilo sambamba na
yakini ya kumcha mungu na kutegemea malipo yake.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba kufunga
mwezi wa mtukufu wa ramadhani kwa waumini ni kutekeleza kwa vitendo elimu ya nidhamu katika kiwango cha juu cha mafunzo yatokanayo
na ramadhani na kwamba waumini kuacha vyakula vya halali kwa kumuogopa mola wao na kutarajia fadhila za mwezi mtukufu
wa ramadhani ni jambo kubwa ambalo waumini wanapaswa kuliendeleza hata baada ya
mfungo wa ramadhani.
Mhe. Othman amesema kwamba ni vyema
kwa waisalamu wote kuiendeleza nidhamu inayopatikana katika mwezi mzima wa
ramadhani ili wananchi na waislamu kwa jumla waoneshe kuhitimu kwao mafunzo
yaliyopatikana mwezi wa ramadhani na elimu hiyo iweze kuwa na manufaa zaidi duniani na kesho
akhera.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mgharib
Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa akitoa salamu za mkoa baada ya futari hiyo, ameitaka jamii kukemea maovu yaliyomo ndani
ya maeneo yao hasa sauala ya kuwepo
madanguro na upigaji wa muziki bila
kufuata taratibu jambo ambalo ndio chachu ya maovu mengi kutokea na linaleta
kero kubwa kwa wananchi na waumini na
wananchi mbali mbali..
Mhe. Kitwana amesema kwamba mwezi
huu wa ramadhani ni mwezi wa kuchuma kheir na kujifunza zaidi kusoma ili itoe
nguvu ya kuweza kuyaona mabaya zaidi na kuweza kujipendekeza kwa Mwenyezi Mungu
Muumba kupata fadhila njema.
Amewataka wananchi kushikamana na
kupendana kwa wema na kukumbushana katika mema na kuachana na mabaya na kuwaomba
wananchi wote wa kukema vitendo vya ushoga ambavyo vimekuwa vikishamiri kutokana na kuhamasishwa
sehemu nyingi duniani .
Amewataka wananchi wa Zanzibar kupambana kwa kukema
suala la vitendo vya namna hiyo unaotangazwa na baadhi ya mataifa duniani na
kutaka wananchi wote walaani na kwamba viongozi kwenye mitaa wasiruhusu kuwepo madanguro na upigaji wa madisko bila
kufuata taratibu na maelekezo ya
serikali.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kutopitia Kitengo chake cha Habari leo tarehe 01.04.2023.
No comments:
Post a Comment