Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman O. Kinana ameongoza Ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo na Mhe. Vo Van Thuong, Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Jijini Ha Noi, Viet Nam.
Katika mazungumzo hayo, Ndg. Kinana aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, wa kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizo mbili ili kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Vietnam.
No comments:
Post a Comment