Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Uwekezaji, Viwanda na Biashara, TRA pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Jijini Dar es Salaam

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Kikao Maalum na Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Waziri wake Dkt. Mwigulu Nchemba, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakiongozwa na Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na Kamishna Mkuu Alphayo Kidata pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka. Kikao hicho kimefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.