Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Amefungua Jengo Jipya la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Ikulu Mpya Chamwino Dodoma kuhudhuria hafka ya ufunguzi iliofanyika leo 20-5-2023.
Taaswira ya Jengo jipya la Ikulu ya Chamwino kama linavyoonekana pichani ambalo limezinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Ikulu Mpya Chamwino Dodoma kuhudhuria hafka ya ufunguzi iliofanyika leo 20-5-2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino huku viongozi mbalimbali wakishuhudia katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzindua Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wakipiga ngoma kabla ya kuingia Rasmi katika Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuingia Ofisini kwake Chamwino Mkoani Dodoma mara baada ya uzinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Jengo Jipya la Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, lililofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Jengo Jipya la Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, lililofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said akiwa Viongozi wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Jengo Jipya la Ikulu Chamwino Dodoma lililofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, (kulia) Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo, Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaaf Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Viongozi wengine wakihudhuria hafla hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Mama Maria Nyerere wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Hayati Rais wa Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mama Janeth Magufuli wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Viongozi wa Serikali, Viongozi wastaafu, wa kwanza kushoto Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mstaaf wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi,wakiwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu Chamwino. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.