Habari za Punde

Wazee Watakiwa Kushirikiana katika Kuwaelimisha Vijana Kuwaenzi Watoto Ndio Nguzo Muhimu Katika Jamii.

Na.Maulid Yussuf. 

Mkurugenzi Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee bwana Hassan Ibrahim Suleiman amewaomba wazee kushirikiana katika kuwaelimisha vijana wao juu ya kuwaenzi watoto kwani ndio nguzo muhimu katika jamii. 

Akifungua mafunzo ya Mfunzo ya Mabaraza
ya Wazee juu ya umuhimu wa kuwatunza wazee katika jamii katika ukumbi wa mikutano  Sebleni kwa wazee, amesema vijana kuwatunza wazee kunawafanya nao pia kutunzwa na watoto wao wakati nao wtakapozeeka.

Amewaomba wazee kuyatumia vizuri mafunzo wanayopatiwa ili iwe chachu ya kuwaenzi wazee katika jamii inayowazunguka.

Mapema Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Wazee Bikame Sheha Ussi, amesema lengo la mafunzo hayo ni kukumbushana juu ya umuhimu wa kuwatunza wazee kwa mabaraza hayo ya wazee ili nao kusaidia kuwaelimisha na wengine katika shehia zao.

Amewaomba washiriki kuwa ni mabalozi wazuri wa kuelimisha wengine katika jamii, ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa.

Akiwasilisha maada ya Wazee, Afisa Wazee kutoka Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee bi Pili Mussa Saadala amesema mzee ana umuhimu mkubwa katika Jamii hasa katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Wakitoa michango yao juu ya haki za wazee, baadhi ya washiriki wamesema wazee wana haki ya kupatiwa elimu, kushirikishwa katika vikao vya ushauri pamoja na kupatiwa unafuu wa nauli za usafiri pamoja na kupewa fursa katika sehemu mbalimbali za kijamii, kiuchumi, na kuwezeshwa.

Aidha wameshauri kua inapotokea misaada kwa wazee ni yema kufikiriwa wazee wa vijijini zaidi kuliko wazee wa sebleni na  welezo, kwani wao wapo katika uangalizi mzuri wa Serikali kuliko  wazee wa vijijini.

Hata hivyo wamekemea na kulaani tatizo la baadhi ya vijana kuwaita wanga au wachawi wazazi wao au wazazi wa wenzao pamoja  na kutowatenganisha wazee wao endapo mmoja wao atapata maradhi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamewashirikisha   mabaraza ya wazee kutoka shehia mbalimbali.

MWISHO

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA UHUSIANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.