RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki Mhe.
Iddi Seif Bakari, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiwa katika mazungumzo na mgeni wake
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uturuki Mhe.Iddi Seif Bakari
(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kuja kumuaga
akielekea katika Kituo chake cha Kazi Nchini Uturuki, mazungumzo hayo
yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu
Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Iddi Seif Bakari
aliefika kwaajili ya kumuaga.
Alisema, Urutuki ni taifa lililoendelea
kiuchumi ikiwemo sekta viwanda na kuimarika miundombinu yake, hivyo alimtaka
Balozi huyo kuisimamia vyema sera ya Dilopomasia ya uchumi kwa kuangalia fursa
ya uwekezaji wa viwanda kuja nchini kuwekeza badala ya kutegemeza zaidi bidhaa
kutoka huko.
Aidha, alimtaka Balozi huyo
kuwashajihisha wafanyabiashara wa Uturuki kuja Tanzania ikiwemo Zanzibar
kufungua viwanda vya uzalishaji wa bidhaa zinazopendwa zaidi na Watanzania
wengi.
Akizungumzia sekta ya utalii, Rais Dk.
Mwinyi alimtaka Balozi Seif kuweka mkazo zaidi kwa kulishajihisha shirika la ndege
la Uturuki linalofanya safari zake za moja kwa moja nchini, kuutangaza Utalii
wa fukwe, Mji Mkongwe pamoja na mbuga za wanyama zilizopo nchini kwa kuwa na
matangazo mengi ya utalii kwenye ndege za shirika hilo.
Dk. Mwinyi pia alimshauri Balozi Iddi
Bakari kuwavutia wawekezaji wa miundombinu ikiwemo bandari, barabara na viwanja
vya ndege ili kuimarisha maendeleo ya sekta hizo.
Kwa upande wake, Balozi Iddi Bakari
alimuahidi Dk. Mwinyi na Watanzania kwa ujumla kuzitumia vyema fursa za uchumi ziliopo
Uturuki kwa kuzipatia soko bidhaa za Tanzania likiwemo zao la pamba ambapo
Uturuki ina mahitaji makubwa ya malighafi ya pamba kwa viwanda vya uzalishaji
nguo nchini humo.
Mbali na kuahidi kuutangaza vyema
utalii wa nchini, Balozi Bakari aliahidi kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania
TTB pamoja na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar kutoa matangazo mengi kwa Shirika
la ndege la Uturuki pamoja na kuimarisha uhusiano wa diplomasia nchini humo
kuleta watalii wengi zaidi.
Sambamba na hilo, pia alieleza mikakakti
ya kuimarisha ushirikiano na Uturuki kwa kuangalia uwezekano wa ndege ya mizigo
ya ATCL kufanya safari zake nchini humo kwa kuboresha uhusiano wa biashara
kwenye sekta ya usafirishaji wa mizigo na vifurushi baina ya Tanzania na
Uturuki.
Balozi Iddi Seif Bakari aliteuliwa na
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa balozi
wa Tanzania nchini Uturuki Aprili 05 mwaka huu, kabla ya uteuzi huo alikuwa, Konseli Mkuu nchini Dubai.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment