Na Rahma Khamis Maelezo
Wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar wametakiwa kuchukua juhudi za makusudi ili kuhakikisha Sheria ya Chuo inakuwepo Chuoni hapo ili wanafunzi ,Maafisa na wananchi waweze kuifahamu.
Akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Magereza juu ya kuwaongoza wanafunzi wanawake huko Ofisini kwao Magereza Mhadhir wa Sheria Chuo Kikuu cha Zanzibar University (SUZA) Dkt Sikujua Omar Hamad amesema kukosekana kwa sheria hiyo imepelekea kuwakosesha baadhi ya haki za wanafunzi waliopo chuoni hapo.
“Tumebaini kuwa sheria na kanuni za Chuo cha Mafunzo hazipatikani ipasavyo kwani hata wao wenyewe hawazifahamu sheria hizo, hivyo fanyeni marekebisho ya sheria ili mupate kuifahamu kwani bila ya kanuni hakuna sheria”,alisisitiza Mhadhir Sikujua.
Amesema Sheria ya Chuo cha Mafunzo haijulikani hata kwenye mitandao jambo ambalo linapelekea kufanya makosa kwa badhi ya Maafisa bila kujua hivyo ipo haja ya kufanya kila jitihada ikiwemo kufika Baraza la Mapinduzi kuhakikisha sheria hiyo inapatikana na kutumika .
Aidha Mhadhir amefahamisha kuwa mafunzo hayo yamelenga zaidi kujua miongozo ya Kitaifa, Kimataifa na Kikanda katika kuwasimamia wanawake wa Chuo cha Mafunzo kutakakopelekea Maafisa wa magereza kujua vipi watawaongoza watuhumiwa na wanafunzi ambao wapo Chuoni hapo.
Mhadhir ameeleza kuwa Mataifa ya nchi nyingi yamepiga hatua juu ya sheria ukilinganisha na sheria za huku jambo ambalo linarejesha nyuma jitihada za kimataifa katika kuwezesha wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo kupata haki zao.
Nae Afisa anaesimamia Miradi ya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia kutoka (TAMWA) Zainab Salum Abdalla amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakufunzi kufahamu namna gani wanaweza kuwasimamia wanawake waliomo katika Gereza kwa kuzingatia miongozo na sheria.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kupata uwelewa wa kujua mambo mengi ikiwemo haki ya michezo na Ujasiriamali kwa wanafunzi wao lakini wanashindwa na nyenzo za kufanikisha kupatikana kwa haki hizo.
Hivyo wameiomba Serikali kuwasadia nyenzo zikiwemo za michezo ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapata haki yao ya ya kucheza kwani kuna baadhi ya maswala hawawezi kuyafanikisha bila ya kupata usaidizi.
Mafunzo hayo ni ya siku mbili yameandaliwa na Chama cha Waaandishi wa Habari Wanawake TAMWA kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo
No comments:
Post a Comment