Na Maelezo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Omar Ali Yussuf amekabidhi vifaa vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 27 kwa idara ya katiba na msaada wa kisheria iliyopo chini ya Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora.
Akikabidhi Msaada huo huko Ofisini Kwake Maisara Mjini Zanzibar alisema lengo la msaada huo ni kuwasaidia watoa huduma za kisheria kuweza kutatua matatizo mbali mbali ya kisheria katika jamii sambamba na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Akitolea ufafanuzi wa msaada huo Mkurugenzi huyo amesema kukabidhi vifaa hivyo ni urejeshaji wa huduma kwa jamii na kutekeleza ahadi ya mamlaka hiyo waliyoitoa katika kilele cha siku ya wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika katika Ukumbi Wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil Kikwajuni hivi karibuni.
Alieleza kuwa mamlaka imetoa jumla ya Printer kumi na moja,Laptop tano na Vishkwambi viwili kwa wasaidizi wa kisheria wa Wilaya kumi na moja za Unguja na Pemba ili kurahisha kazi zao.
Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Hanifa Ramadhan Said ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na
Nishati Zanzibar (ZURA) kwa kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili watoa hudua za msaada wa kisheria .
Awali wahudumu hao walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zililizokua zikirejesha nyuma utendaji wao wa kazi hivyo msaada huo utasaidia kutatua changamoto hizo katika utendaji.
Watoa huduma za msaada wa kisheria ni wafanya kazi wa kujitolea ambao wamekua wakifanya kazi kubwa ya kusaidia jamii kuweza kupata haki zao kisheria.
No comments:
Post a Comment