Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akagua Mabanda mbalimbali kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu kuhusu Tume hiyo inavyowasaidia wakulima wenye ubunifu mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwanzilishi wa Kampuni ya Avomeru Bw. Jesse Oljange kuhusu ukamuaji wa mafuta mbalimbali ikiwemo ya zao la parachichi katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mhandisi wa Mtaani (Street Engineer) Adam Zacharia Kinyekile kutoka Tunduma Mkoani Songwe jinsi alivyobuni na kutengeneza mashine hiyo ya kuvuta maji, kupukuchua mahindi kusaga nafaka pamoja na kubeba Mizigo wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane ambapo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Vijana waliohitimu Mafunzo ya Elimu ya Juu na kujiingiza kwenye masuala ya Kilimo na kuelezea jinsi walivyofanikiwa kwenye Sekta hiyo katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa AVOAFRICA Tanzania Ltd Nagib Karmali kuhusu namna alivyoitikia wito wa Rais Samia kuja Tanzania kuwekeza kwenye Kilimo cha Parachichi katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.