Habari za Punde

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale atembelea maonesho ya Nne ya wiki ya Elimu Zanzibar

 


Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohamed Said amesema maonesho ya 4 yataleta mafanikio makubwa kwa Wanafunzi wengi kujua namna ya kujiunga na fani zenye soko la ajira duniani.
Amesema hayo wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya Nne ya wiki ya Elimu Zanzibar huko Maisara Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema uwepo wa taaluma ambayo itasaidia Wanafunzi kujua vipaombele vya Serikali ili taifa lizalishe wataalam wazalendo.
Amesema kumekua na utitiri wa vyuo hivyo kupitia maonesho hayo yatasaidia jamii kuweza kutambua chuo sahihi na kuweza kijiunga.
Maonesho hayo ya Nne yameshirikisha zaidi ya vyuo 57 kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.